Rais wa Afrika Kusini Bw. Jacob Zuma anakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye kutoka kwa viongozi wa chama chake cha ANC.
Zuma amenusurika mara kadhaa katika kura za kutokuwa na imani naye bungeni, lakini hii ni mara ya kwanza kwa chama cha ANC kumjadili.
Chombo Kikuu cha ANC kimeongeza muda wa mkutano wake kujadili hoja ya kutokuwa na imani naye iliyowasilishwa na Waziri wa Utalii, Derek Hanekom.
Rais Zuma amekuwa akiendelea kushutumiwa kuhusiana na tuhuma za rushwa, huku ripoti ya hivi karibuni ikimhusisha na familia ya kitajiri ya Gupta.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT