
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.
Katika
miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa,
wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa
“darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa
Wasomi
wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha
mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari
mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!).
Hii inachangiwa na mambo mawili:-

I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli
Wasomi
wengi kwa sababu ya “mentality” ya kuogopa kukosea huwa hawapendi
kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa
kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato
lao la uhakika

II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!
Katika
maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa
sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa
kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.
Simaanishi
kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya
kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani;
ukakileta huku mtaani.
Mwandishi maarufu wa vitabu vya uhamasishaji motivational books katika kitabu chake maarufu cha Rich Dady, Poor Dady anauliza swali hili:
“Does School prepare children for the real life” ni swali la msingi sana tunalopaswa kujiuliza hapa. Na pia katika kitabu hicho hicho anasema:
“Get with the times! Look around the richest people didn’t get rich because of their Education”
Mtaani
panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri
ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.
Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze jinsi gani wamefanikiwa.
Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze.
Endelea
kunufaika kutoka kwa Bepari wako kila siku kwa kutembelea ukurasa huu
na kupata mapya yatakayokujenga zaidi. Pia hakikisha unashea ukurasa huu
kwa wenzio usiwe mbinafsi, usinufaike peke yajko. Siku iwe njema kwako
na karibu tena.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT