Madhara ya tatizo la mkojo mchafu (uti) | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 15 Novemba 2016

Madhara ya tatizo la mkojo mchafu (uti)

Karibu tena ndugu yangu wa damu katika ykurasa huu leo tuokoe afya zetu. Afya ndio mtaji wako wa kwanza katika shughuli yoyote inayokuweka mjini iwe biashara, ajira, kilimo,elimu, nk hivyo uonapo mada inayohusu afya unatakiwa kuipa kipaumbele cha kwanza kuisoma kuliko hata inayohusu pesa. Katika mada ya leo nitazungumzia juu ya Mkojo mchafu na madhara yake. Karibu tuwe wote.
Image result for uti
Mkojo mchafu (UTI) ni matatizo katika njia ya mkojo ambayo huchangiwa na maradhi na matatizo ya aina mbalimbali.
Matatizo ya UTI husababishwa na vimelea (bacteria) ambavyo huingia katika njia ya mkojo. Ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote pasipo kujali ni mwanaume au mwanamke.
Hata hivyo mwanaume huweza kuhisi dalili za UTI mapema zaidi kuliko mwanaume hii ni kutokana na tofauti za kimaumbile.
Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hususani katika mfumo wa njua ya mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwea na vimelea.
Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi ukilinganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bacteria huweza kupata urahisi wa kuingia ndani.

Chanzo cha UTI
Tatizo hili husababishwa na vyanzo mbalimbali, lakini zaidi ni maambukizi yanayosababisha UTI ni 'e.coli' na vijidudu vingine vya magonjwa ya zinaa mfano (klamidia) na vijidudu vya kisonono.
Virusi ambavyo husababisha tatizo hili ni kama vile 'herpes simplex' na 'cytomegalo virus' mbali na sababu hizo nyingine ni pamoja na kushiriki ngono na wanawake wanaume/ wanawake wengi kwa upande wa wanawake pia ni mojawapo ya chanzo cha tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Wengine wanaopatwa zaidi na tatizo hili ni wale wenye tabia ya kufanya ngono au kuwaingilia wengine kinyume na maumbile.
 
Dalili za UTI
Dalili zake zinatofautiana kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume mwenye tatizo hili anaweza kukojoa mkojo wa njano sana kila wakati na unakuwa na harufu mbaya hata na wakati mwingine mkojo huambatana na damu.
Mwanaume anaweza kutokwa na manii kwenye mkojo au anapojikamua haja kubwa, huhisi muwasho katika njia ya mkojo na ukiminya uume unahisi unauma na wakati mwingine unakuwa umevimba.
Uume pia hulegea au unaposimama huuma, vile vile hupata maumivu unapotoa manii wakati wa tendo, lakini manii huweza kuambatana na damu.
Athari kubwa kwa wanaume ni kupunguza nguvu za kiume na kuziba njia ya mkojo.
Kwa wanawake wao hushambuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu na na moto wakati wa haja ndogo, homa za mara kwa mara na kutetemeka.
Wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi kama ni malaria au taifodi, lakini pia myu mwenye UTI huisi kukojoa mara kwa mara pamoja na nyonga zote kuuma na kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na muwasho.
Hata hivyo, ulaji wa tunda la tikiti maji kwa wingi huweza kusaidia kusafisha njia ya mkojo na kusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utajipatia tiba bora na kutapata kupona tatizo hilo bila shaka. 

ukijenga utamaduni wa kutembelea ukurasa huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT