Msanii wa zamani wa muziki wa asili Saida Karoli amedai yeye anasikia
kama watu wengine kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond ameiangia
mkataba na meneja wake wa zamani kuhusu kutumia vionjo vya nyimbo zake
katika kutengeneza wimbo ‘Salome’ wa Diamond.
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo
zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye
hilo.
“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi
nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga
ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na
kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja
wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na
hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala
hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili
aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”
Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.
Diamond na uongozi wake baada ya kuachia wimbo huo, walionyesha picha wakati wakifanya makubaliano na meneja wa zamani wa Saida.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi
wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili
kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya
publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata
percent,” Diamond alikiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT