Kwa mara ya kwanza mtangazaji wa kike mwenye vazi la hijab ataruhusiwa
kutangaza habari kwenye kituo cha televisheni nchini Canada.
Ginella Massa ambaye ni mwanahabari wa kike wa Canada mwenye asili ya
Panama na anayejitanda hijab, aliarifu kwamba atakuwa akisoma habari za
usiku katika kituo cha televisheni ya CityNews.
Massa alitoa tangazo hilo kupitia ujumbe aliousambaza kwa kutumia akaunti yake ya mtandao wa jamii wa Facebook.
Massa pia alifahamisha kuridhishwa na uamuzi huo kwa kuwa hapo awali
hakukutokea mwanamke yeyote wa hijab aliyewahi kutangaza habari.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT