Wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi ya taifa ya serengeti
wilayani Bunda mkoani mara,wamelazimika kuangua kilio wakati
wakimwelezea naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi jinsi
wanavyokabiliwa na njaa kali baada ya makundi makubwa ya tembo kuvamia
makazi ya watu na kula chakula kilichohifadhiwa katika maghara huku
wakiharibu sehemu kuba ya mazao mashambani.
Baadhi ya wananchi hao kijiji cha kihumbu wilayani bunda,wametoa kilio
hicho katika mkutano wa hadhara mbele ya naibu waziri huyo wa
kilimo,mifugo na uvuvi mh william ole nasha huku wakiomba serikali
kuwapa chakula cha msaada pamoja na kuangalia namna nzuri ya kudhibiti
makundi hayo makubwa ya tembo.
Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Bi.Yidia Bupilipili,akizungumza wakati
akitoa taarifa kwa kuhusu hali chakula kwa kiongozi huyo,amesema wilaya
ya Bunda inakabiliwa na njaa kali hasa baada ya makundi hayo ya tembo
kuharibu zaidi ya tani mia tano za chakula mashambani.
Hata hivyo naibu huyo kilimo,mifugo na uvuvi Mh. William Ole
Nasha,akizungumza na wananchi wa kijiji hicho,pamoja na kutoa pole kwa
wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo ya taifa ya Serengeti
na mapori ya akiba ya Ikorongo kutokana na athari hizo zinazosababishwa
na makundi hayo ya tembo,lakini pia amesikitishwa na idara ya
wanyamapori kushindwa kutoa fidia kwa wananchi ambao wamekubwa na tatizo
hilo,hatua ambayo amesema imesababisha uhasama mkubwa kati ya wahifadhi
na jamii.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT