Bukoba. Wakati baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wakilalamikia kukosa misaada iliyotolewa na wahisani kwa wathirika wa tetemeko la ardhi, imedaiwa kuwa Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM imekarabatiwa kwa fedha hizo.
Madai hayo yalitolewa na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronikus Karumuna kuwa sehemu ya miundombinu ya shule hiyo yakiwamo mabweni yalikarabatiwa ili kupokea baadhi ya wanafunzi waliohamishwa kutoka sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo zinajengwa upya.
Akichangia taarifa ya tetemeko la ardhi iliyowasilishwa jana katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera (RCC), Meya huyo alishutumu matumizi mabaya ya fedha hizo. Alisema haikuwa haki kutoa kipaumbele cha ukarabati wa shule inayomilikiwa na CCM badala ya sekondari za Serikali.
Meya huyo alisema kamati ya maafa kushindwa kuzishirikisha kamati za mitaa na kata kumesababisha malalamiko mengi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT