Aidha wamempa wiki mbili meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa shinyanga kuwapatia bima zao ambazo tayari zimeshaiva na kwani ni haki yao ya msingi.
Hayo yamesemwa na katibu wa cwt wilaya ya meatu james msimba ngĂombe wakati wa hafla ya kuwaaga walimu wastaafu 20 wa mwaka 2015 na 2016 na kuwapa mkono wa kheri .
Amesema kuwa walimu wastaafu wamekuwa wakidahalilishwa na waajiri wao pale wanaposhindwa kuwapa malipo na nauli ya kufunga mizigo ya kurudi makwao ,wengi wamefukuzwa katika nyumba walizokuwa wakiishi ,hivyo wamemuomba mkurugenzi atekeleza malipo yao kabla ya walimu hao kuanza kuhesabu fedha za kujikimu za kila siku.
Akizungumza katika hafla hiyo katibu wa cwt mkoa wa simiyu said mselem amesema kuwa kustaafu sio mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mazuri ,hivyo amewaasa kabla ya kupata hundi zao ni vema wakaiweka fedha hiyo katika akaunti na kufikiria mradi wa uzalishaji ili fedha iweze kupata mzunguko huku akiwasisitiza kuwekeza hisa katika benki ya walimu
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT