Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu
za serikali za Mitaaa (LAAC), Vedasto Ngombare Mwiru, katika taarifa
yake kuhusu hesabu zilizokaguliwa na kamati ya hesabu za Serikali za
Mitaa kwa mwaka 2013/2014 na 2014/2015.
Katika mradi huo uliokuwa ujengwe eneo la Gongo la Mboto Halmshauri ya
Jiji la Dar es Salaam, iliwekeza kupitia kampuni ya nyama iliyoianzisha
ya East Africa Meat Company Ltd, lakini mradi huo haukuweza kufanyika
kwa kiasi cha pesa kilichopangwa.
Aidha kati taarifa hiyo imeonesha maeneo 10 nyenye matatizo sugu ya
matumizi ya fedha za serikali za Mitaa, ikiwemo eneo la manunuzi
yasiyozingatia sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT