Msanii mkongwe wa muziki nchini, Matonya amedai hakuna kinachoshindikana
kama wasanii, viongozi pamoja wadau mbalimbali kwa pamoja wakiamua
kuwapatanisha Alikiba na Diamond.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sugua Benchi’, ameiambia
Bongo5 kuwa maelewano kwa wasanii ni kitu ambacho kitaleta tija na
msingi mzuri kwa wasanii pamoja na jamii inayowazunguka wasanii.
“Chuki ndo chanzo cha mambo mengi ambayo yanatokea katika hii dunia,”
alisema Matonya “Kama unakumbuka katika kipindi cha nyuma kuna wasanii
walichomana visu na mmoja akafariki sitaki kulizungumzia kiundani lakini
nadhani watu wanaelewa nazungumzia nini,”
“Wasanii wote ni kitu kimoja, tunatakiwa kuungana kwa pamoja ili
kuupeleka muziki wetu sehemu fulani, kwa hiyo mimi nadhani kuwapatanisha
Diamond na Alikiba haishindikani, tuna viongozi wengi, wasanii kwa
pamoja tunaweza kuwaweka sawa na hata wakafanya project ya pamoja,”
aliongeza Matonya.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT