Habari ya leo ndugu yangu mwana mwanamafanikio mwenzangu na karibu sana katika mtandao wetu huu ambao ni darsa la bure kabisa katika nyanja tofauti za maisha yetu. Katika upande wa mafanikio leo nakuletea mada Je, Unafahamu Una Uwezo Sawa na Hawa Watu? Karibu ujifunze kitu na tubadilishe maisha yetu kwa pamoja.
Nashangazwa sana na uwezo wa binadamu. Huwezi kusema huyu atakuja kuwa hivi kwa sababu ya kumwangalia machoni.
Kuna watu wengi sana wamefikia mafanikio kwa kutokea sehemu ambazo hazitegemewi. Wengine hukumbana na majanga au hatari kubwa sana lakini bado huweza kufikia mafanikio makubwa sana.
Wapo waliozaliwa wakiwa na udhaifu fulani lakini bado wameweza kufikia mafanikio makubwa!
Suala la kufanikiwa linawezekana kwa mtu yeyote aliye katika hali yeyote, haijalishi kazaliwa akiwa na kilema au udhaifu gani. Bado unaweza kuutumia udhaifu wako ukawa faida kubwa sana kwako.
Kama wewe hujasoma unaweza kuutumia udhaifu wako wa kutosoma, kufikia mafanikio makubwa sana.
Kama wewe umesoma lakini hujapata ajira itumie hiyo nafasi kama fursa na itumie kufikia mafanikio makubwa.
Kwa kuwa mafanikio ni haki ya kila mtu kama zilivyo haki nyingine ebu na wewe weka malengo ya kuweza kufikia mafanikio. Tofauti kati ya haki yako ya mafanikio na haki nyingine ni kwamba haki ya mafanikio haidaiwi kama tunavyodai haki nyingine, mafanikio unayatafuta mwenyewe.
Ebu fikria kuhusu kijana kama Diamond, huyu ameweza kufanya makubwa katika tasnia ya muziki na sasa ni maarufu sana Afrika na duniani. Au Samata ambaye pia amefanya vizuri sana katika tasnia ya mpira wa miguu mpaka sasa anacheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Kuna mtu mwingine anitwa Mwalimu Nyerere, huyu katoka familia ya kikulima mpaka kufikia hatua ya kuikomboa nchi ya Tanzania.
Hivi unajua kwamba unaweza kuwafikia hawa kimafanikio? Je, unafahamu una uwezo sawa na hawa watu? Kwa haraka unaweza kusema hapana.
Sasa nimekuchukua mtaani kwako na nimekukutanisha na mtu ambaye anafanya kibarua, hana nyumba na maisha yake hayajakaa vizuri.
Je, unafahamu kwamba una uwezo sawa na huyo mtu. Jibu la haraka linaweza kuwa namzidi.
Zamu hii nimekuleta kazini kwako. Sasa tunakutana na wafanyakazi wenzako na watu wa karibu kazini kwako. Nikikuuliza je, u ajua kwamba una uwezo sawa na hawa watu? Bila shaka utaniambia ndio au utasema nawazidi kidogo.
Baada ya hapo twende mpaka Daresalaam na hapo nakukutanisha na mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi.
Je, unafahamu kwamba una uwezo sawa na Reginald Mengi?
Bila shaka utaniambia hapana.
SOMA: Tabia ya Kusikiliza inavyoweza kubadilisha maisha yako usivyotarajia!!
SOMA: Tabia ya Kusikiliza inavyoweza kubadilisha maisha yako usivyotarajia!!
Kwa nini?
Ni kwaida ya binadamu. Huwa tunaangalia matokeo ya sasa ya mtu na kudhani atakuwa hivyo siku zote. Kama hajafanikiwa basi tunadhani atabaki vivyo hivyo siku zote.
Je, kuna ukweli kuhusu hili?
Hili suala sio kweli. Hii inatokana na ukweli kwamba uko ulivyo kwa sababu ya kile unachokifikria .
Kwa hiyo kama utapanua akili na mawazo yako na kuona kwamba unaweza kufikia mafanikio ambayo yamefikiwa na mtu yeyote yule unaweza kuyafikia haswa. Usijiwekee ukomo wa kufikiri na kutenda. Unaweza kuwa kama mtu yeyote yule ambaye unamwona amefikia mafanikio.
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT