Muuza nyago kwenye video za nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva, Gift
Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kumtia hasira na kumchefua staa wa sineza
za Kibongo, Wema Isaac Sepetu baada ya kukutana ukumbini kwenye
bethidei ya meneja wa wasanii wa muziki.
Ubuyu wa motomoto ulidai kuwa, baada ya kukutana, Gigy alidaiwa kucheza
muziki kihasarahasara na mmoja wa ‘mazilipendwa’ wa Wema, jambo ambalo
mlimbwende huyo hakupendezwa nalo.
Ishu hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Hyatt Regency The
Kilimanjaro Hotel uliopo Posta jijini Dar ambapo mastaa kibao walikuwa
wageni waalikwa kwenye shughuli hiyo iliyotawaliwa na mavazi ya
kizamani.
Kwa mujibu wa shushushu wa Wikienda aliyekuwa ndani ya shughuli hiyo,
awali Wema alionekana mwenye bashasha tele akiwa na wapambe wake, lakini
Gigy alipoanza makeke yake ndipo bibie huyo akapoa kama maji ya mtungi.
“Mwanzoni Wema hakuwa na tatizo kabisa na Gigy, lakini baada ya
mwanadada huyo kwenda kucheza kihasara na zilipendwa wa Madam (Wema)
hapo ndipo balaa likaibuka, akanywea na kumkata jicho la hasira, hata
wale wapambe wake (Wema) wakaanza kumvimbia Gigy baada ya kuona anataka
kuharibu shangwe za mama la mama.
“Gigy alionekana ni mwenye furaha tele, kwani alikuwa amepiga maji ya
kutosha (pombe) hivyo hakujali hata kidogo kama anamkwaza mtu, isitoshe
kilichoharibu zaidi ni baada ya jamaa kunogewa na manjonjo ya Gigy na
kumzawadia wigi lake alilokuwa amevaa,” aliongeza sosi.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Wikienda lilimtafuta Gigy na kumuuliza
kulikoni kumkera Wema kwa kumchezea vibaya bwana wake wa zamani ambapo
bila hiyana alifunguka:
“Ni kweli nilicheza na huyo mtu tena kwa kujinafasi kwa sababu ilikuwa
ni sehemu ya furaha, sikuona sababu ya kujivunga eti kwa sababu
nitamuudhi Wema au mtu yeyote yule.
“Kwanza yeye ameshaachana naye kitambo kama bado ana wivu naye atajijua mwenyewe,” alisema Gigy.
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa na hata alipotumiwa chatting kupitia WhatsApp zilionesha
kupokelewa lakini hakujibu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT