Msanii Afande Sele amefunguka mengine mapya kwa kudai shindano la Miss
Tanzania kwa sasa linatia aibu kubwa katika taifa kwa kukosa hadhi huku
likionekana ni shindano linalomnufainisha mtu mmoja nasiyo taifa kama
ilivyokuwa awali.
Afande Sele amesema hayo baada ya watu wengi ndani na nje ya nchi
kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania 2016/2017, Diana
Edward kwa wakidai limechakaa na linashusha hadhi ya mashindano hayo
pamoja na kuvunja moyo kwa watu ambao walikuwa na lengo la kushiriki
katika mashindano mengine yajayo.
“Utapeli ni nini ?....Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss
Tanzania 2011 zinatoa jibu la swali hilo…Lakini pia ni vyema tukamuomba
waziri husika katika masuala hayo …a.k.a Dk. Marufuku akamuulize
muandaaji wa Miss Tanzania kama ni kweli ameaumua kuzeeka labda hata
kufa na shindano lake?”. Ameandika Afande Sele kupitia mtandao wake wa
kijamii Instagram
Msanii huyo aliendelea kwa kusema “Kama kweli iko hivyo basi itoshe pia
kubadili jina la shindano kwa kuliita Miss jina lake badala ya kuendelea
kutia aibu Taifa kwa kuliita Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya
kitaifa katika maeneo yote kwa makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja
tu…aibu yake aibu yetu…Imetosha sasa…imestosha sana”.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT