
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), imesema hali ya vipindi vifupi vya mvua
katika maeneo ya mwambao wa pwani ya Kaskazini itaendelea hadi Mei 9.
Taarifa ya tahadhari iliyotolewa na TMA jana inasema kunatarajiwa kuwapo
vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam na Pwani. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imesema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini.
“Wakazi wa maeneo tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua
stahiki. Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila
itakapobidi,” imesema taarifa ya TMA.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT