Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema barua
ambayo amemuandikia Rais John Magufuli, bado haijajibiwa.
Lissu alisema ni muda mrefu walimwandikia barua Rais Magufuli kutaka
kukutana naye kwa ajili ya uongozi mpya kujitambulisha rasmi kwake na
kufanya naye mazungumzo.
“Tunasubiri ajibu barua yetu kwa kuwa tulishaomba kukutana na Rais Magufuli tuzungumzie utawala wa sheria,” alisema Lissu.
“Tunafahamu yuko busy (ana shughuli nyingi), lakini atenge muda hata
nusu saa au saa nzima ya kuongea na kiongozi wa chama cha mawakili wa
Tanganyika,”
Alisema lengo kubwa ni kujitambulisha na kuzungumzia utawala wa sheria
na mwelekeo wa Taifa. Pia, ana imani kwamba Rais atawakaribisha.
Kiongozi huyo wa wanasheria alisema watakachokifanya ni kumweleza maoni
ya TLS na pale watakapoona amekosea, hawatasita kumweleza na anapoona
kuna matatizo awe huru kuwaeleza. Alisema Rais akikubali itakuwa ni
vizuri kwa sababu ni maongezi ya kawaida kwa lengo la kuimarisha TLS na
kujitambulisha kwake.
Lissu, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki alichaguliwa kuwa rais
wa chama hicho mwezi uliopita na Rais ni mmoja kati ya viongozi kadhaa
ambao TLS imewaandikia kuomba kukutana nao.
Aliwataja wengine kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Kaimu Jaji Mkuu,
Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wawili wastaafu; Benjamin Mkapa na
Jakaya Kikwete. Amesema tayari Kaimu Jaji Mkuu ameshakubali ombi lao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

0 comments:
POST A COMMENT