
VIONGOZI zaidi ya 20 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata na
matawi Jijini Arusha wamesimamishwa uongozi kwa tuhuma za kufuja mali za
chama.
Kata ambazo viongozi wake wamesimamishwa kwa tuhuma hizo za ubadhirifu
ni Unga Limited, Themi, Sekei, Sombetini na Daraja Mbili. Viongozi hao
ni wenyeviti, makatibu, wachumi na makatibu wenezi.
Katika kata ya Unga Limited, mbali ya viongozi wa kata kuchukuliwa hatua
pia viongozi wa matawi wa wamesimamishwa kwa madai ya kushindwa
kusimamia ipasavyo mali za chama.
Mbali ya tuhuma za kufuja mali za chama, baadhi ya viongozi hao pia
wanatuhumiwa kufanya hujuma katika chaguzi zilizopita, ikiwa ni pamoja
na kuficha fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania uongozi ili wao waweze
kuwania tena nafasi hizo na kupita bila ya kupingwa ama kuwa na wagombea
dhaifu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Katibu wa Uenezi na
Itikadi wa CCM, Humphrey Pole pole alisema na kutoa salamu kwa
watendaji wote wa chama hicho kote nchini kuhakikisha wanatunza mali na
kuzitumia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Polepole alisema katika baadhi ya maeneo mali za chama zinatafunwa kama
mchwa na viongozi mbalimbali hivyo msako unaendelea kote nchini kuwasaka
na bila ya kuonea mtu.
Katibu huyo alisema chama hakiwezi kuwavumilia viongozi wanaofuja mali
kwa sasa chini ya uenyekiti wa Rais John Magufuli. "Wote watachukuliwa
hatua kali," alisema.
"Kuna baadhi ya maeneo mali za chama zinatumika vizuri sana... kuna
baadhi ya maeneo mengine viongozi wanafuja vibaya lakini wameachwa.
"Kwa sasa hilo halipo.
"Heri kuwa na viongozi wachache waaminifu na waadilifu wenye kufuata
katiba ya chama kuliko kuwa na utitiri wa viongozi wezi na wasiokuwa
waaminfu. Hilo haliko kwa sasa chini ya uongozi wa (Rais) Magufuli."
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT