
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa
Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa akiugulia afya
yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya
nchi kupatiwa matibabu.
Polepole amezungumza na AZAM NEWS ambapo alisema tangu Mzee Kinana akiwa
hata kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya.
“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa
kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo
ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na
anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini, shambani
moja kwa moja inashauriwa kitaalam atumie muda wa kupumzika ili
kuimarisha afya yake na nimezungumza nae anaendelea vizuri yuko
madhubuti kabisa kuliko jana,” alisema Polepole.
Katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT