
Madaktari wa Hospitali ya Aga Khan na Prince Aly Khan nchini India,
wanatarajia kuboresha huduma za upasuaji wa mifupa na majeraha kwa
kutumia mtandao wa What’sApp.
Teknolojia hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutumika nchini baada ya
madaktari bingwa kutoka India kuwasili. Madaktari hao kutoka Hospitali
ya Prince Aly Khan waliwasili nchini jana kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa
wenzao wa Hospitali ya Aga Khan kutumia teknolojia hiyo ya kisasa
kufanya upasuaji.
Daktari bingwa wa upasuaji mifupa na majeraha wa Hospitali ya Aga Khan,
Harry Matoyo amesema madaktari hao walioanza upasuaji wataondoka
Jumatatu na kwamba, wanatarajia wataalamu wa hospitali hiyo watakuwa
wamenufaika na uzoefu watakaopata.
“Tumetengeneza group (kundi) la What’sApp ambalo litatumiwa na madaktari
bingwa wa upasuaji mifupa kati ya nchi hizi mbili, kwa ajili ya
kusaidiana iwapo tutakwama wakati wa upasuaji. Tunaweza kupiga picha na
kuuliza kitu kinachotakiwa kufanyika,” alisema Dk Matoyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT