
Mfumo mpya wa matumizi ya namba za simu (Number Portability) unatarajiwa
kuanzishwa ifikapo Machi Mosi kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) na kampuni za simu nchini.
Kampuni za simu zilizoingia katika mkataba huo ni pamoja na Tigo, Vodacom, Airtel, TTCL, Zantel, Smile, Smart na Halotel.
Jana, TCRA ilitangaza huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa simu nchini,
itakayomwezesha mteja kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine na kuendelea
kutumia namba yake ya awali.
Mpango huo tayari umeshatekelezwa kwenye nchi nyingi za Ulaya na hata Afrika Kusini.
Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi, Musa Aziz amesema
pamoja na faida zilizopo bado kuna hofu kwa watumiaji kutokana na
usumbufu wa mawasiliano.
“Nafikiri kutakuwa na gharama za ziada mimi nikimpigia mwenzangu sitajua
kwa wakati huo anatumia mtandao gani, hapo ninaweza kuingia gharama
kubwa zaidi, sina hakika kama italeta unafuu japokuwa ni mpango mzuri,”
amesema Aziz.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT