
Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu kama
Diamond Platinumz kuonekana kukiuka Sheria za Usalama Barabarani,
ametozwa faini ya Sh60,000 katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Usalama
Barabarani kwa makosa mawili ya kutofunga mkanda na kuachia usukani
wakati akiendesha gari lake akiwa na familia.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema
walimuita Diamond baada ya kuona kipande kifupi cha video kwenye mtandao
wa Instagram.
“Alitii wito na alikuja juzi ila nilikuwa na kazi nyingi sikuweza
kuonana naye na leo (jana) aliweza kufika tena tukaonana, akalipa faini
na tukamuonya kufanya kitendo kile alihatarisha maisha ya familia yake,”
amesema Mpinga.
Mpinga amesema kutokana na umaarufu wake ndani na nje ya nchi kitendo
hicho kingesababisha mashabiki wake kumuiga na kusababisha ajali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT