
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Rich Mavoko amedai maisha ya WCB ni mazuri
na anaishi na wasanii wenzake kwa upendo na kushirikiano ingiwa
migongano haikosi.
“Kusema kweli maisha ni mazuri sana, tunaishi kwa upendo,
tunashirikiana, ni sehemu ambayo unaweza ukakaa na kufanya muziki nzuri
kwa sababu watu ambao wanakuzunguka ni wasanii hata mabosi wetu, Sallam
na Tale ni watu ambao wako kwenye huu muziki wa muda mrefu,” alisema
Rich Mavoko.
Kwa upande wa muziki wake muimbaji huyo amedai mpaka sasa ameona
mafanikio makubwa katika muziki wake hasa hasa kimataifa zaidi kwa kuwa
nyimbo zake nyingi zinachezwa kimatifa.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake
kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kolabo zake za kimataifa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT