Dar es Salaam. Maisha ya JKT Ruvu na Majimaji katika Ligi Kuu Bara
yanategemea na jinsi zitakavyoweza kuchanga vyema karata zao kwenye
mechi zao tisa zilizobakia kabla ya ligi hiyo kumalizika.
Hata hivyo, ratiba ya ligi hiyo huenda ikawa msumari wa moto kwa timu
hizo mbili katika kipindi hiki kigumu zinapopambana kuhakikisha zinabaki
kwenye ligi.
JKT Ruvu wenye pointi 16, watacheza mechi sita ugenini na tatu watakuwa
uwanja wa nyumbani kati ya mechi tisa walizonazo mkononi.
Hali itakuwa mbaya zaidi kwa maafande hao iwapo watashindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya Mbao FC.
Baada ya mchezo huo, JKT Ruvu itakabiliwa na mechi nne mfululizo
zinazofuata kwenye viwanja vya ugenini ambako huwa nadra sana kwa timu
ngeni kupata ushindi.
Maafande hao watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar, Prisons, Mwadui FC
na Kagera Sugar. Kufanya vibaya kwenye mechi hizo kuna maanisha kuwa
JKT Ruvu itajiweka kwenye nafasi finyu ya kubakia Ligi Kuu.
Kama ilivyo kwa JKT Ruvu, Majimaji nayo pengine kwa sasa itakuwa inajuta
kwa kushindwa kutumia vyema faida ya kuwa na mechi nyingi uwanja wa
nyumbani kwenye mzunguko wa kwanza.
Baada ya kufungwa na Simba mwishoni mwa wiki iliyopita, Majimaji sasa
itakabiliwa na mechi tatu mfululizo zinazofuata dhidi ya Stand United,
Mbao FC na Kagera Sugar.
Wakati Majimaji na JKT Ruvu zikiwa na jukumu zito la kuhakikisha
zinaibuka na ushindi kwenye mechi mfululizo za ugenini, wapinzani wao
katika vita ya kubakia Ligi Kuu, Ndanda FC, Toto Africans na African
Lyon zenyewe zinapumua kwani zina ratiba inayowabeba kwa kutolazimika
kwenda kucheza mechi nyingi za ugenini mfululizo.
Kocha wa JKT Ruvu, Bakari Shime alisema bado wana nafasi ya kubaki Ligi Kuu licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu mbele yao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT