Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa
72), imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Suleiman ‘Morocco’
kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000 (laki tano).
Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Makocha. Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi, hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.
Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu mwingine wowote.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT