MAENEO USIYOYAJUA YANAVYOATHIRI UTU WAKO WA NDANI | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 7 Februari 2017

MAENEO USIYOYAJUA YANAVYOATHIRI UTU WAKO WA NDANI

Habari yako mpenzi msomaji wa blog hii. Bila shaka u mzima wa afya. Mimi mzima ndiyo maana asabuhi hii nimeamka na kukuletea makala hii kama ilivyo utaratibu wangu niliyojiwekea. Natumaini unaendelea kupata maarifa muhimu sana katika safari yako ya kukamilisha ndoto/maono yako.

Bepari na rafiki yako leo ninapenda kuja na mada tajwa hapo juu ili uweze kujua ni vitu gani vinavyoweza kuharibu mtindo wako wa kufikiri. Mada hii imelenga kukusaidia kukujengea mtizamo chanya ili ufikie katika malengo yako. Huwezi kufikia malengo yako huku unaendelea kujiachia hovyo katika baadhi ya mambo. Tukubaliane kila kitu kina miiko yake. Uwezi kuwa mwana muziki mkubwa, au mwigizaji mkubwa, au mfanya biashara mkubwa au mwandishi mkubwa wakati unaishi maisha ya kawaida kabisa. 

Ukiona unaishi maisha ya kawaida kabisa kama jamii inayokuzunguka inavyoishi, uwe na hakika na wewe utakuwa na maisha ya kawaida kama wao. Ni lazima utambue kuwa maisha yenye mafanikio ni tunda la mabadiliko makubwa ya kimtizamo utu wa ndani. Kila mtu ana ndoto/ maono makubwa kama wewe lakini ishu kubwa ni namna gani anafikia lengo hilo. Sasa wewe walau umeanza kuchukua hatua ni lazima uonyeshe utofauti, lasivyo nawe kuwa tayari kuwa kama wao. 
Unaweza kutumia mfano mdogo sana, ebu jaribu kufuatilia hata kwa watu wachache tu mwenye mafanikio wanavyoishi. Unaweza kuanza kwa kufuatilia unaoishi nao, utagundua utofauti wa maisha wanayoishi na wewe.
 Utagundua ni watu wanaojali sana muda. Ni watu wanaofanya kazi kwa bidii kubwa, ni watu wanaoamka mapema sana. Au mara nyingine utawaona wakiwa katika shughuli nyingi nyingi, mpaka kuna muda unajiuliza huyu au yule mbona haridhiki? Anaangaikia nini na utajiri mkubwa alionao?

Huo ni mfano mdogo, au pengine hujanielewa vizuri. Kama ulisoma shule, ulionaje mienendo ya waliokuwa wakifanya vizuri darasani. Wewe ni shahidi mara nyingine utawakuta hawalali mapema wanasoma, au utawakuta wakati nyie mnapiga stori wao wako bize wanasoma; wakati mwingine utawaona ni wadadisi wa mambo, hivyo muda mwingi watautumia kukaa karibu na walimu ili waelekezwe. Kwa ujumla unaweza kuona utofauti wao na wewe, basi hiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kuwa bora kuliko wewe/nyie. Yaani wakati wewe unaishi kikawaida wao waliishi kiutofauti na ndiyo maana wakawa tofauti na wewe. Kwa lugha nyingine ni kwamba “Utavuna ulichopanda”.

Sasa kwa mifano hiyo hapo juu utakuwa mahala pazuri pakutambua kitu kimoja kikubwa kwamba utofauti huo ulikuwa ni mitizamo yenu. Yaani namna mlivyokuwa mnachukulia mambo ndani yenu ndiyo sababu kubwa ya utofauti huo. Ina maana muonekano wenu wa nje ni matokeo ya utu wenu wa ndani. Na mara nyingi utu wenu wa ndani umeathiriwa zaidi na malezi na mazingira uliyokulia.

Nimeyasema haya kama utangulizi lakini, usiogope! Maana unafuatilia makala zetu ili upate suluhisho. Na mimi nakuhaidi suluhisho utalipata; sasa nikwambie siri ya ajabu sana katika maisha yako ni kwamba  mawazo hukupelekea kutenda, matendo huleta mazoe, mazoea hutengeneza tabia, tabia hukuletea hatma yako”. Ukitaka kuwa na hatima njema ni bayana, lazima uingilie kati hiyo cheni ya hatma yako. Kwa kujilazimisha kufikiria mambo kama unavyotaka. 
Tabia ulizonazo sasa ndizo zinazokufanya leo uwe ulivyo sasa. Tabia za uvivu, uzinzi, uongo, kucheza na muda, kuona mafanikio ni bahati, kutukana, kutumia muda vijiweni, kutokupenda kusoma, na kadhalika zote hizo ndizo zimekufanya uwe ulivyo sasa. Kwa kifupi tabia ni ujumla wa mazoea yako kila siku. Kila kitu ukifanyacho kwa kujirudia kinakuwa ni mazoea, mazoea hayo ndiyo yanayozaa tabia yako. Ni jukumu lako kujikondisha ili uwe na tabia nzuri, tabia za kimafanikio, tabia za kiushindi. 
Swali, je unawezaje kujikondisha? Hilo ndilo somo letu.

Pamoja na kuendele kukuletea maarifa mbalimbali ya namna ya kubadilika kimtizamo(utu wa ndani), katika makala hii nitakusaidi kuepukana na mazingira yanayoathiri mtizamo wako. Na haya mazingira yanaleta ukinzani mkubwa sana wakati unachukua hatua za kubadili tabia zako. Na wengi hamju kama mazingira hayo yanakukwamisha. Makala hii inalenga pia kukufanya uwe mbali na mazingira hayo ili ufanikishe mabadiliko uyatakayo.
 Yafuatayo ndiyo mambo yanayokufanya uwe na tabia ulizonazo sasa ambazo ndizo zinazokukwamisha kufikia mtizamo, matendo, mazoea, na tabia ulizo nazo sasa. Na mara nyingine unaweza kuwa unajua au hujui:-

Mazingira Unayoshinda. Mazingira tunayoshinda kila siku na kwa muda mrefu yana nafasi kubwa sana kuamua aina ya tabia ulizo nazo. Hapa namaanisha watu tunaoshinda nao wanaweza kuwa marafiki, wafanyakazi wenzako, ndugu au jamaa zako. Pia stori tunazozizungumza. Mazingira hayo ndiyo yanayojenga mtizamo wako na kupelekea matendo,mazoea na tabia yako. Na mara nyingine hili linafanyika bila wewe kujua, kwa sababu ubongo wako wa ndani (Subconscious Mind) hubeba kila kitu bila kuchuja na hatimaye kinakuja kukuathiri katika maamuzi yako.
Nasema hivi sina maana ya wewe kujitenga na jamii ili kukwepa hili, la hasha! Nataka uchukuwe tahadhari hasa aina ya mazungumzo ya kushiriki, jenga tabia ya kuwa bize ukifanya shughuli zako, na kama unataka kuchanganyika basi tenga muda. Lakini hata katika muda huo ulioutenga chunga aina ya mazungumzo utayoshiriki. Kwa sababu kama utakubali kusikiliza mazungumzo yenye ushawishi hasi uwe na hakika yatakuadhiri tu. Kama ni kazini epuka mizaa isiyo na maana, fanya kazi kwa bidii, epuka kuongea hovyo hovyo. Hakuna faida yoyote utayopata katika mazungumzo hayo ya hovyo. Onyesha utofauti na tegemea matokeo chanya.


 Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!


Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT