Baada ya kuja na operesheni ya kupambana na dawa za kulevya, jina la
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda linaweza kuwa ndilo
lililotajwa zaidi katika mkutano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na
kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki ya pili sasa.
Makonda alianza kuwa mjadala ndani na nje ya nchi baada ya kutaja orodha
ya kwanza na ya pili ya watu maarufu wakiwamo wasanii, wanasiasa na
viongozi wa dini na kuagiza wafike Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam
wahojiwe kuhusu dawa za kulevya.
Kasi ya kutajwa kwa jina lake iliongezeka zaidi Jumatano iliyopita baada
ya kumtaja Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe,
Askofu Josephat Gwajima na mfanyabiashara Yusuf Manji.
Hata hivyo, Mbowe, Gwajima na Manji wamekanusha vikali kuhusika na
biashara hizo na kuahidi kumshtaki Makonda kwa kashfa. Gwajima na Manji
wameshahojiwa polisi.
Katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums, hadi kufikia juzi saa 8:00
mchana, kulikuwa na kurasa 49 ambazo jina la Makonda lilikuwa limetajwa
mara 961 katika mijadala iliyokuwa ikiendelea.
Mijadala hiyo ilikuwa ikihusu kama Makonda yuko sahihi au la katika
utaratibu alioutumia na kama ana mamlaka ya kuagiza watu kuripoti
polisi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT