Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye
ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya
hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata
faida.
Kwa muda kulikuwepo na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kumsainisha
msanii huyo mkongwe kwenye label ya WCB. Na sasa, ingawa hajasema kuwa
amepanga kumsanisha kwenye label hiyo, Diamond amekiri kuwa kwenye
mipango ya kufanya kazi na legend huyo.
“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu
kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na
bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza
mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.
“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji
mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania
watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.
Naye Q-Chief alisema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika
kwasababu ni mtu ambaye ameniita kwa ushauri nikiwa na QS, amemuambia
vitu vingi vya msingi, yeye shahidi hapa, lakini kama ni mtu anayeelewa
mdogo wake ameniita amesema nini mpaka mimi nimeelewa na hajafanya maybe
[QS] is not ready to do business but Diamond is a business man and I am
ready to join a business man so long as kuna misingi. Lakini naamini
ngoma inayofuata Diamond amenipa baraka zake.”
Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila
amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda
anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa
ilioufanya kwake.
Ndugu zake pia walihoji kuhusu mkataba wa maisha aliosainishwa mtoto wao
kwenye kampuni hiyo na kwamba tangu awe chini ya kampuni hiyo hawajaona
mabadiliko ya maana kwenye maisha yake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT