Wanafunzi zaidi ya 500 kutoka chuo cha Kampala waliokosa mikopo wakusanyika wizara ya elimu. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Wanafunzi zaidi ya 500 kutoka chuo cha Kampala waliokosa mikopo wakusanyika wizara ya elimu.

Wanafuzi zaidi ya mia tano wa fani mbalimbali kutoka chuo cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam waliokosa mikopo wamekusanyika wizara ya elimu sayansi na teknolojia kwa lengo la kupata kauili ya serikali juu ya hatima yao huku wakihoji uhalali wa vyuo vingine kupata mikopo kwa asilimia 80 lakini wao ni asilimia tano tu.

Wakizungumza wizarani hapo baadhi ya wanafunzi hao wamedai kuwa licha ya kuishi mazingira magumu pia hawawezi kujilipia ada ambayo ni zaidi ya milioni sita na kwamba wanashangazwa na kitendo cha bodi ya mikopo awali kuorodhesha kuwa wapo kwenye orodha ya wanaostahili kupata mkopo lakini baadae wakawaondoa.

Serikali licha ya kuwataka kufuata utaratibu wa kuwasilisha madai yao imewaeleza kuwa wanaostahili kupata mkopo ni watoto yatima ambao hawana baba wala mama na kuwaahidi kwenda kuzungumza nao huko chuoni ili kuona namna ya kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo wanafunzi hao wameelza kutokuridhishwa na majibu ya serikali kwa madai kuwa serikali iliahidi kuwa itatoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili hasa ambao wazazi hawana uwezo.

Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi lililazamika kuimarisha ulinzi katika jengo la wizara hiyo.

Source: Itv
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT