Mkuu huyo wa wilaya,Mohamed Utaly ametoa agizo hilo ikiwa ni siku chache baada ya kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba ambapo Mvomero imeingiza shule mbili za Chohelo na Magunga kati ya kumi zilizo shika mkia ikiwa ni pamoja na shule ya msingi chohelo sambamba na magunga iliyo katika kata ya Maskati ambapo amesema udanganyifu huo umefanya shule nyingi kushindwa kufanya vyema kitaaluma.
Nao wadau wa elimu wa wilaya ya Mvomero wamekiri hali mbaya ya uhaba wa walimu katika maeneo yao kuchangiwa na viongozi kushindwa kutimiza wajibu wao na kwamba kauli ya mkuu huyo wa wilaya ikifanyiwa kazi kiutendaji badala ya siasa itasaidia watoto wengi vijijini kupata elimu sawa na mijini huku Mkurugenzi wa wilaya ya Mvomero Florent Kyombo pamoja na kuahidi kusimamia maagizo hayo ameahidi adhabu kali kwa walimu watakao bainika kughushi vyeti.
Wakati wa zoezi la utangazaji wa matokeo ya darasa la saba kimkoa,Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk John Ndunguru amewaagiza Maafisa elimu kuwafuatilia walimu wanaoacha kufundisha na kujiingiza kwenye siasa,kwani sababu hiyo,uwafanya wanafunzi wengine kujiingiza kwenye biashara ya bodaboda,vigodoro na ngoma za asili hali inayochangia kufanya vibaya katika matokeo hayo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT