| Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 3 Desemba 2016

 SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameweka wazi kutopendezwa na kitendo cha Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuendelea kuzaa nje ya ndoa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ akisema kuwa ni kinyume na maadili na sheria za dini ya Kiislam.

Shehe Salum aliyasema hayo juzi Alhamisi (Novemba 1, 2016) alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa, Amani na Risasi zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar na kuzungumza na waandishi pamoja na wafanyakazi wa idara nyingine.


Akijibu swali la Mwandishi Aziz Hashim aliyetaka kujua dini inasemaje kuhusiana na watu kama Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa, shehe huyo alisema:
“Niseme tu kwamba hili si kwa Diamond na Zari tu bali kwa wote wanaofanya zinaa. Dini ya Kiislam inaeleza kuwa, kuzini ni dhambi. Hivyo kitendo cha Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa hatakuwa na tofauti na wanyama wengine ambao nao wanazaliana bila kufunga ndoa.
“Tofauti ya binadamu na wanyama kama mbuzi, ng’ombe au nguruwe ni kwamba, sisi tunatakiwa kuzaliana baada ya kufunga ndoa, kinyume chake tutakuwa tunapata dhambi.
“Halafu sasa tukio la kufunga ndoa wala halichukui muda mwingi na halina gharama kubwa. Ni suala la wahusika kumtafuta tu shehe, anakuja anatia ubani kisha mnaendelea na maisha yenu. Kama ni kutumia pesa itakuwa ni elfu hamsini tu au laki moja.
“Labda niseme tu kwamba, hata mimi kama kweli wamedhamiria kufunga ndoa, niko tayari kuwaozesha bure kabisa, nitaweka gari yangu mafuta kuwafuata popote, wao wajipange tu wakiwa tayari wanitafute.”
Shehe huyo aliongeza kuwa, anaona litakuwa jambo jema kwa wawili hao kuoana kwani kuendelea kuzaa nje ya ndoa ni kuwakosesha haki watoto wao hasa ile ya kurithi mali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT