Wachina hawataki utani wanamtaka Messi, wamemtengea zaidi ya Tsh Bilioni 220 | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Ijumaa, 16 Desemba 2016

Wachina hawataki utani wanamtaka Messi, wamemtengea zaidi ya Tsh Bilioni 220

Ni siku kadhaa zimepita baada ya taarifa za staa wa Arsenal Alex Sanchez kuhitajika na timu za China huku wakitaja kumshawishi na mshahara mnono, leo December 16 Lionel Messi wa FC Barcelona ameripotiwa kuhitajika na timu ya Hebei China Fortune FC ya China.
Hebei China Fortune wanamuhitaji Lionel Messi ambaye mkataba wake na FC Barcelona unamalizika 2018, Hebei China Fortune wameishangaza dunia baada ya kutajwa kuwa watakuwa wapo tayari kumlipa Messi mshahara wa euro milioni 100 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 220.
Kama Lionel Messi akikubali kujiunga na Ligi hiyo atakuwa ndio mchezaji pekee duniani mwenye mshahara mkubwa ambapo kwa wiki atakuwa akilipwa zaidi ya Tsh bilioni 4.7, Barcelona ambao wamemuongezea mkataba leo Luis Suarez, wamepanga kumuongezea na Messi na watakuwa wakimlipa euro milioni 35 kwa mwaka.
Hebei China Fortune tayari ina mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa duniani Ezequiel Lavezzi, lakini timu hiyo ina mastaa wengine waliowahi kutamba Ulaya kama Stephane Mbia, Gael Kakuta na Gervinho wanaofundishwa na kocha wa zamani wa Man City Manuel Pellegrini .
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT