Vikwazo vya biashara Rwanda,Tanzania kuondolewa | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 7 Desemba 2016

Vikwazo vya biashara Rwanda,Tanzania kuondolewa

SERIKALI ipo katika majadiliano na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Rwanda ili kuona uwezekano wa bidhaa zinazotoka ndani ya nchi hizo kutokaguliwa tena kama nchi mojawapo itakuwa imeshakagua.

Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage katika mkutano wa kibiashara baina ya Tanzania na Rwanda.

Ngonyani alisema ili kufikia katika uchumi wa viwanda, ni lazima kuondolewa kwa vikwazo vyote ili kukuza viwanda ambavyo vinakubalika katika nchi hizo.

Alisema katika mkutano huo watajadiliana kuona jinsi taasisi za nchi hizo zinaweza kufanya kazi moja, na kuondoa usumbufu unaolalamikiwa na wafanyabiashara wao.

“Kwa mfano taasisi kama TBS (Shirika la Viwango Tanzania) inayokagua ubora wa bidhaa Tanzania ikishak
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT