Kama
ilivyo kawaida, kazi yangu ni kuhakikisha haupitwi na chochote, na leo
nimeipata hii kutoka kwa Kim Kardashian ambaye ni mke wa rapa Kanye West
anayedaiwa kuanza mipango ya kufungua kesi ya madai ya talaka dhidi ya
mume wake huku akitaka mahakama impe haki kamili ya malezi ya watoto wao
wawili.
Huenda
ikakushangaza hii kwasababu ya kile kinachofahamika kuwa rapa Kanye West
hayuko sawa kiafya kwasasa baada ya kulazwa Hospitali siku chache
zilizopita kutokana na kudaiwa kuwa na msongo wa wa mawazo pamoja na
uchovu mwingi.Kwa
mujibu wa mtoa taarifa ambaye inaelezwa kuwa ni rafiki wa karibu wa Kim
amesema kuwa pamoja na magumu anayoyapitia rapa huyo, Kim ameamua
kuanza mipango ya kudai talaka ikiwa ni siku chache baada ya ripoti ya
Daktari kueleza kuwa Kanye West asikae karibu na silaha ya aina yoyote.
Taarifa zilizotolewa na mtandao wa Us Weekly zimeeleza
kuwa Kim anakamilisha kesi ya madai ya talaka ambayo itampa haki zote
za kulea watoto wao wiwili North mwenye miaka mitatu pamoja na Saint
ambaye ametimiza mwaka mmoja Jumatatu ya wiki hii Dec, 5. 2016
“Japokuwa
itachukua muda mrefu sana kulitekeleza hilo, lakini Kim hahitaji tena
kuendelea na ndoa yake. Na hili linatokea wakati ambao Kim amekuwa
msaada mkubwa kwa mume wake ambaye yuko kwenye matatizo ya kiakili
kwasasa, lakini bado ameonesha kutotaka watoto wake wakae karibu na
Kanye” – Rafiki wa Kim
Mapema
wiki hii iliripotiwa kuwa Kim na Kanye watangana kutoka kuishi nyumba
moja na sasa kila mmoja anaishi kivyake na hii ni baada tu ya Kanye
kuruhusiwa kutoka Hospitali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT