Aidha tangu uhakiki wa watumishi hewa uanze hadi sasa serikali imebaini watumishi hewa zaidi ya 17,000 ambao walikuwa wakilipwa fedha huku wengine wakiwa wamestaafu na wengine kufa.
Akizungumza na wananchi waliofurika Uwanja wa Barafu uliopo eneo la Mto wa Mbu Wilayani Monduli Mkoani Arusha jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema serikali imetenga fedha hizo kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme kwa wananchi wake.
Alisema wazabuni watasaini mikataba yao ya kufanya kazi hiyo ya usambazaji wa umeme vijijini Desemba 15 mwaka huu na kazi kuanza mara moja ili kufungua fursa za ajira katika sekta mbalimbali nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo, William ole Nasha alisisitiza kuwa serikali itaendelea kutoa elimu kwa wafugaji ili wabadilike pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazao ya chakula ili kuepuka baa la njaa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT