Serikali yavitaifisha viwanja 15 vilivyokuwa vinamilikiwa na raia wa Uingereza. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 6 Desemba 2016

Serikali yavitaifisha viwanja 15 vilivyokuwa vinamilikiwa na raia wa Uingereza.

Serikali imevifutia hatimiliki viwanja 15 vilivyokuwa vinamilikiwa na raia mmoja wa uingereza na kuvitaifisha viwanja hivyo vilivyopo katika mikoa ya Kanda ya ziwa.

Uamuzi wa kufuta hatimiliki za viwanja hivyo vilivyokuwa vinamilikiwa na mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Hermant Patel mwenye uraia wa Tanzania na Kenya, umetolewa na Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh. William Lukuvi ambaye amesema raia wa kigeni haruhusiwi kumiliki ardhi kwani ni kinyume cha taratibu na sheria za nchi.

Mh. Lukuvi ameongeza kuwa, awali serikali ilikuwa ikifahamu kwamba mfanyabiashara huyo anahatimiliki ya viwanja vitano lakini baada ya uchunguzi uliohusisha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza, umebaini raia huyo ana hatimiliki za viwanja kumi na vitano.

aidha Waziri Lukuvi amewatupia lawama baadhi ya watumishi wa wizara yake kwa kutokuwa makini katika usimamizi mzuri wa utoaji wa hati za umiliki ardhi kwa raia wa kigeni kitendo ambacho amekikemea na kuwataka kubadilika.

Baadhi ya viwanja vilivyofutiwa hatimiliki na kutaifishwa na serikali ni pamoja na kiwanja namba 98 kitalu ' F' Nyakato Mwanza, kiwanja namba 45 Mkuyuni Mwanza, viwanja namba 539 na 560 kitalu 'A' Magongo Geita.

Kiwanja namba 113 kitalu 'A' Nyamongoro Mwanza, kiwanja namba 798 Magongo Geita,kiwanja namba 529 Magongo-Geita,viwanja namba 531 na 532 Bombambili Geita na viwanja namba 533 na 534 kilichopo mjini Geita.

Viwanja vingine ni kiwanja namba 332 kilichopo Bwiru Ilemela Mwanza,kiwanja namba 330 kitalu 'A' Bwiru Ilemela Mwanza, kiwanja namba 115 Nyamhongoro Mwanza,kiwanja namba 3 kitalu 'C' kilichopo Lamadi Busega mkoani Simiyu na kiwanja namba 1 na 2 vilivyopo Lamadi - Busega mkoani Simiyu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT