Meya Dar asema Kupandisha tozo za maegesho siyo dhambi | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 7 Desemba 2016

Meya Dar asema Kupandisha tozo za maegesho siyo dhambi

 Isaya Mwita - Meya wa Jiji la Dar es Salaam
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amejitokeza na kutolea ufafanuzi uamuzi wa halmashauri hiyo kupandisha tozo za maegesho ya magari, na kusema kuwa uamuzi huo siyo dhambi kwa kuwa ulikuwa ni muhimu kufanyika kwa sasa.
Tozo hizo za maegesho ya magari katika maeneo ya katikati ya jiji zimepanda kutoka shilingi 300 hadi shilingi 500 kwa saa moja.

Mwita amesema kutokana na mahitaji makubwa ya fedha za kuliboresha jiji hilo, ni muhimu wakazi wake wakachangia michakato mbalimbali ya maendeleo kupitia nyongeza hiyo ya shilingi 200 za kitanzania.

Akitolea mfano wa miradi inayopaswa kufanyika katika jiji hilo, Mwita amesema kuna tatizo kubwa la mipango ya ujenzi, (Master Plan) ambalo amepanga kulimaliza ndani ya miaka miwili.
 Maegesho mtaa wa samora DSM

"Siyo dhambi kuongeza shilingi 200 kwenye tozo za maegesho kwa kuwa ni fursa kwa wakazi wa jiji hili kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo, kubwa likiwa ni master plan, Jiji la Dar es Salaam halina master plan, wote tunalalamika kuwa halijapangika, sasa mimi niliyepewa dhamana ya kulisimamia nina jukumu kubwa la kuhakikiksha jiji hili lina kuwa la mfano" Amesema Mwita.

Akizungumzia suala la machinga, Mwita amesema anaunga mkono uamuzi wa Rais Magufuli wa kuamuru machinga waachwe mjini hadi watakapopatiwa maeneo mengine yenye biashara na kwa upande wa jiji lake tayari wameshaandaa eneo la Mbezi ambalo litakapokamilika, litatumiwa na wafanyabiashara hao.
Kariakoo DSM
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT