Binti wa Kitanzania, Jennifer Shigholi ameibuka kuwa Mjasiriamali katika Bara la Afrika(African Enterprenuership Awards) katika Mashindano yaliyofanyika Desemba 5 Nchini Morroco.
Shigholi amewahasa Vijana kuendelea kudhubutu na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini ilikuweza kujikomboa kichumia na badala yake kuacha kulalamika na kuchukua hatua za uthubutu kwa kuwa kila kitu kinawezekana kama mtu akimua.
Pia amesema kuwa Serikali imempatia eneo la kujenga Kiwanda kikubwa zaidi ilikuweza kutoa ajira kwa vijana hapa Nchini.
Hivyo hivyo Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF Salum Shamte, amesema Mjasiliamali huyo ameleta heshima kubwa katika nchini yetu na sisi kama Sekta binafsi tutafanya naye kazi bega kwa bega ilikumsaidia kuweza kuendeleza biashara zake.
" Jennifer ni Mfano wa kuigwa na Vijana wengine kwa Ujasiliamali wake Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania inampongeza kwa Ushindi wake kwenye tuzo za Ujasiliamali barani Afrika na kuiletea nchi yetu heshima kubwa haswa wanawake" amesema
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT