Msanii wa miondoko ya mduara AT jana kabla ya kutolewa kwa tuzo za
#EATVAwards aliweka nadhiri kuwa endapo msanii Alikiba akishinda kwenye
tuzo hizo kwa furaha basi yeye atakojoa kitandani na kuposti picha ya
tukio hilo.
Baada ya kuweka nadhiri hiyo usiku wa jana Alikiba aliibuka na ushindi
kwa kubeba tuzo tatu na kufanya kuwa msanii wa kwanza katika tuzo hizo
kuchukua tuzo nyingi kwa wakati mmoja, hivyo baada ya ushindi huo AT
alikamilisha ahadi yake ya kukojoa kitandani na kuweka picha kama
uthibitisho wa furaha aliyonayo baada ya mkali Alikiba kuibuka na tuzo
tatu.
Mbali na hili AT amesema kwa sasa yeye yupo likizo katika muziki hivyo hawezi kutoa kazi yoyote mpaka mwakani na kusema yeye na Alikiba ni kati ya wasanii wakali wenye uwezo wa kutunga nyimbo kali na kukaa muda mrefu pasipokuwa na nyimbo na wakafanya poa pindi wanaporudi.
"Bado nipo likizo hadi 2017 kama msanii wako mkali aimbe nyimbo kama 'Nipigie au Makimuga' hadi leo zipo na uhai hadi miaka 50 ijayo. wakati mwingine mashabiki muwe wazima wa akili timamu kufuatafuata mkumbo kwenu siku moja kutawatia kiharusi kuna wasanii hawawezi kukaa hata mwezi kimya ulizeni kwanini? Anaejiamini haogopi wingi wa wasanii anaogopa kufanya kitu chini ya uwezo wake". Aliandika AT

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT