Askari wa JWTZ mbaroni kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Askari wa JWTZ mbaroni kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu.

Jeshi la polisi mkoani Manyara linamshikilia askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania John Charles Shadefa wa kikosi cha Land Force kilichopo Kibaha mkoani Pwani akituhumiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu nane kutoka katika Jimbo la Kusini nchini Ethiopia.

 Mwanajeshi huyo alikamatwa na askari polisi katika eneo la kituo cha nishati ya mafuta  cha Mount Meru mjini Babati akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Sienta lenye namba za usajili T 409 mali ya Bw Abdallah Mohamedi Nurdin mkazi wa mtoni  jijini Dar es Salaam akidaiwa kuwasafirisha raia hao.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,Kamanda wa polisi Bw Francis Jacob amesema watuhumiwa hao tisa walikamatwa juzi baada ya kutiliwa shaka na askari polisi waliokuwa kwenye utekelezaji wa majumu wao ya kazi  katika eneo la kituo hicho cha mafuta kilichopo kata ya Maisaka na kuwatia mbaroni.

Aidha Kamanda Jacob akizungumzia mazingira hayo amesema mmiliki wa gari hilo Bw Abdallah Mohamedi Nurdin akiwa na mwenzake walitoroka baada ya kushuka kwenda kuwanunulia chakula na pindi walipobaini kwamba wenzao waliokuwa wamewaacha kwa malengo ya kwenda kuwanunulia chakula tayari wameshakamatwa.

Hata hivyo Bw Jacob amesema polisi wanafanya juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wawili hao ili waweze kufikishwa mahakamani,huku gari hilo likiwa linashikiliwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT