YAMETIMIA...Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Limetangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi Wake | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 23 Novemba 2016

YAMETIMIA...Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Limetangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi Wake

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi wake ikiwa ni njia ya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida na kufikia malengo yake.

Mkurugenzi Mkuu wa shirikia hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi alisema kuwa mchakato wa kupunguza asilimia 90 ya wafanyakazi wa shirika umekamilika na utaratibu wa kuanza kulisuka upya shirika utaanza hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 10 ya wafanyakazi watakaobaki ndio waliokidhi vigezo vinne walivyovitoa ambavyo ni uaminifu, elimu, uzoefu na kujali wateja.

Kwa upande mwingine alisema kuwa wafanyakazi wengine wameenguliwa kwa sababu hawawezi kwendana na kasi inayotakiwa kwa sasa na shirika hilo.

Kwa sasa shirika hilo lina wafanyakazi 221 ambao wanaelezwa kuwa ni wengi kuliko mahitaji halisi. Katika mpango huu wa kupunguza wafanyakazi, wanatarajia kupunguza takribani wafanyakazi 200.

Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na shirika hilo kuwa tayari limewasimamisha kazi takribani wafanyakazi wote katika kituo cha nchini Comoro na kile cha jijini Mwanza.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT