Aina mpya ya mmea usiojulikana unasemekana kumea na kuenea unaosababisha maradhi hasa ya saratani kwa mtu yeyote anayegusa .
Wanasayansi wa Taasisi ya Utafiti ya (TPRI),Taasisi ya Utafiti wa
Wanyamapori (TAWIRI) na taasisi ya elimu kuhusu njaa ECHO wanafanya
utafiti wa pamoja kuhusu mmea huo wa kiajabu kwa jina la 'Parthenium'.
Taarifa zaidi zafahamisha kuwa mtu anapogusa mmea huo huanza kuwa na vipele mwilini.
Aidha utafiti zaidi umeonyesha kuwa mtu anapopumua na kupata harufu ya
mmea huo husababisha matatizo ya kupumua,na kudaiwa kuharibu mapafu na
kusababisha saratani mwishowe kusababisha kifo .
Kwa sasa mmea huo unamea Arusha ingawaje wanasayansi wanasema kuwa pia
unaweza kumea maeneo ya nyanda za juu za Kusini,maeneo karibu na mlima
Kilimanjaro na pia mikoa ya pwani.
Source: trtswahili
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT