Wanafunzi wa kiume wa bweni wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
ya Tweyambe iliyoko wilayani Misenyi, mkoani Kagera wamenusurika kifo
baada ya bweni lao kuungua kwa moto ambao umesababisha hasara kubwa kwa
kuteketeza kabisa mali zote za wanafunzi hao walizokuwa wamezihifadhi
ndani ya bweni hilo ambalo walikuwa wakilitumia kwa ajili ya malazi.
Moto huo ulianza kuwaka kuanzia majira ya saa 2.30 usiku muda ambao
wanafunzi walikuwa kwenye vyumba vya madarasa wakati wakijisomea,
mashuhuda wa moto huo ambao ni pamoja na walimu na wanafunzi, wamesema
moto uliozuka ulikuwa mkubwa sana na ndio maana jitihada za kuuzima
zilizofanywa na kikosi kazi cha jeshi la wananchi kilichoko mkoani
Kagera kwa ajili ya kurejesha katika hali ya kawaida miundombinu
iliyoharibiwa na tetemeko na askari wa kikosi cha zimamoto kwa
kushirikiana na wanafunzi katika shule hiyo zilishindikana.
Nao baadhi ya viongozi ambao ni pamoja diwani wa kata ya Ishozi, William
Rutta na mwenyekiti wa shule ya sekondari ya Tweyambe Habibu Mwijage
wamelihusisha tukio hilo na masuala ya hujuma, wakizungumza wamesema
umeme wa nguvu ya jua ambao umefungwa katika mabweni kuwa hauwezi kuwa
chanzo cha moto uliounguza bweni kama taarifa za awali za uchunguzi wa
jeshi la polisi zinavyoeleza juu ya tukio hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT