Mahakama moja mjini Munich nchini Ujerumani imefungua kesi dhidi ya
muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa kuchochea
hisia za chuki.
Muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg |
Jarida la habari la Ujerumani Der Spiegel limeripoti kuwa kesi hiyo
iliwasilishwa na wakili mmoja wa mjini Würzburg, anayeutuhumu mtandao wa
Facebook kwa kuruhusu wito wa mauaji, vitisho vya machafuko, kukanusha
mauaji ya Wayahudi, miongoni mwa mambo mengine.
Sheria zinazodhibiti maneno ya chuki nchini Ujerumani ni kali, ambapo
ishara za Kinazi na propaganda za kibaguzi zimepigwa marufuku kabisa.
Mtandao huo wa kijamii umekuwa ukishutumiwa mara kwa mara kwa kuchukua
muda mrefu kuondoa habari zenye maudhui yanayokiuka sheria kutoka kwa
tovuti yake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT