Njia za Kupata Faida Katika Biashara Bila Kukwepa Kodi | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 5 Novemba 2016

Njia za Kupata Faida Katika Biashara Bila Kukwepa Kodi


Karibu tena msomaji wangu na tajiri wa kesho mwenzangu, kama ilivyo kawaida yangu kushea na wewe mambo muhimu, leo nakuletea mbinu unazoweza kutumia katika biashara yako kupata faida bila kukwepa kodi na kuepuka rungu la mkuu wa kaya. Karibu tuwe wote.
Lengo la biashara yoyote duniani ni kupata faida toka katika fedha au mali iliyowekezwa. Ili kupata faida katika biashara unayofanya ni lazima ufahamu mambo muhimu katika biashara yenyewe na sheria za biashara katika nchi husika.
Faida ni kiasi kinachobakia baada ya kutoa gharama zote toka kwenye mauzo katika kipindi husika katika biadhaa au huduma ambazo biashara yako inatoa.

Faida= Mauzo – Gharama
Mauzo= Jumla ya fedha zilizopatikana kwa kuuza bidhaa au huduma
Gharama= Jumla ya fedha zilizotumika kuendesha biashara zikihusisha,kununua bidhaa za kuuza,kulipa mishahara wafanyakazi,pango,ada za leseni na gharama nyingine zilizopelekea bidhaa kuuzwa.
Ukiangalia mkokotoo huo hapo juu utagundua kuwa wafanyabiashara wengi wanafanya makosa kwa kutoweka vipengele vingi vya gharama za biashara. Na kwa kufanya hivyo wanafikiri wametengeneza faida kubwa wakati uhalisia ni kwamba si kweli.
Baadhi ya makosa ni kutojumuisha mishahara ya wafanyakazi wamiliki wa biashara. Mara nyingi wafanya biashara ambao wamejiajiri wenyewe katika biashara zao hawajilipi mishahara, au hata kama wakijilipa basi ni kwa kiasi kidogo ambacho kama wangeajiri mtu mwingine kisingetosha.
Ili kujua faida halisi ya biashara yako ni muhimu kujumuisha gharama hizi zote katika gharama za biashara
Ifahamike pia kuwa umuhimu wa biashara si tu kupata faida kwa maana ya fedha bali pia kwa namna nyingine kama kutoa ajira kwa wengine na kwa familia pia kama familia inahusika katika utendaji wa moja kwa moja.

Faida Na Kodi
Kodi ya mapato ni mojawapo ya gharama kubwa na wakati mwingi kikwazo kwa biashara nyingi. Kodi hii inafikia kiwango cha asilimia hadi 30 (30%) ya faida kuu.
Kodi ya mapato ni malipo yanayotolewa kwa malaka ya mapato ya nchi kwa faida ambayo biashara inapata.
Faida hii ni kama ile iliyooneshwa katika mkokotoo hapo mwanzoni faida hii inaitwa faida kuu,yaani faida kabla ya kodi.
Hivyo faida kamili ya biashara inapatikana baada ya kutoa gharama na kisha baadaye kutoa kodi ya mapato. Sasa mkokotoo wetu mpya utakuwa kama ifuatavyo:
Faida Halisi= Faida Kuu – Kodi ya mapato
Kodi ya Mapato= 30%* Faida Kuu

Mchanganua wa Mikokotoo hii ni kama ifuatavyo:
Ili kupata faida katika biashara gharama za bidhaa lazima ziwe chini, bei za bidhaa unazouza ziende juu, kodi ya Mapato iwe ndogo. Mada hii inajikita katika namba 3 – Kushusha kodi ya mapato.

Ili kushusha kodi ya mapato ni lazima kuzingatia yafuatayo
Kutengeneza Vitabu vya Kumbukumbu za MahesabuKurekodi na kutunza kumbukumbu zote za miamala ya biashara zikijumuisha manunuzi ya bidhaa,mauzo,na ghrama za uendeshaji kama mishahara,nishati,usafirishaji,leseni n.k. Namba 2 ni muhimu sana kufanyika kwa ukamilifu. Hapa ndipo siri ya mafanikio ya biashara yako.
Kama mfanyabiashara hataweza kuonesha mwenendo wa biashara basi mamalaka ya mapato itamkadiria kodi ya kulipa kitu ambacho si sahihi kwani mara nyingine utakadiriwa zaidi kuliko kiasi cha faida unayotengeneza.
Kama unatumia gari lako binafsi katika kuendesha biashara mfano kusafirisha mizigo toka sehemu moja kwenda nyingine au hata kwenda kazini naa kurudi kama umejiajiri,basi hakikisha umeingiza gharama hizi katika mahesabu.
Gharama nyingine ni zile za benki na leseni mbalimbali,gharama hizi huwa zinasahaulika au wengine hawafikiri kuwa ni gharama za biashara. Kurekodi taarifa zote za matumizi ni jambo moja muhimu sana kukuwezesha kupata faida katika biashara yoyote.
 
Pata Faida Na Ulipe Kodi
Maendeleo ya nchi yoyote yanategemea sana kodi toka kwa wananchi wake na biashara kubwa na ndogo. Hivyo kulipa kodi ni jambo jema kwa mwananchi yeyote kwaajili ya maendeleo ya nchi.
Lakini ni muhimu pia kupata faida katika biashara vinginevyo biashara nyingi zitakufa. Jambo la msingi ni kuwa na mfumo wa kuendesha mahesabu na kutunza kumbukumbu za miamala ya fedha . Hili litasaidia kujua kama umepata faida au umetoa tu huduma kwa jamii.
Kama nilivyosema mwanzoni kuna faida nyingine zaidi ya fedha ya ziada inayopatikana. Unaweza ukawa na faida kidogo au sifuri kabisa, lakini ukwa umetoa ajira kwa watu kadhaa nanhivyo kuboresha hali ya kimaisha kwa wafanyakazi hao na familia zao.
Pia utakuwa umetoa faida kwa kutoa huduma kwa wananchi na hivyo kuboresha maisha yao au biashara zao pia.
Ni matumaini yangu umenufaika na mada ya leo juu ya kupata faida katika biashara na kulipa kodi.
Washirikishe wengine ili wafaidike kama wewe kwa kubofya vitufe vya mitandao ya kijamii chini ya mada hii.

Kama ambavyo umesoma na kunufaika na makala hii naomba na wewe unisaidie kushea na wenzako ukurasa huu kupia facebook, twitter hata whatsapp. Sharing is caring.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT