Ukuaji wa uchumi Tanzania unaridhisha - Utafiti | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatatu, 28 Novemba 2016

Ukuaji wa uchumi Tanzania unaridhisha - Utafiti

Kasi ya ukuaji wa uchumi nchini imekuwa ya kuridhisha katika kipindi cha miaka michache iliyopita, ingawa changamoto imebaki juu ya namna ya kuhakikisha mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji huo inaongezeka.

Hayo yamebainika katika tafiti zinazoonesha kuwa mchango wa kilimo kwemye uchumi umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi inayojishughulisha na tafiti za uchumi ya REPOA Dkt Donald Mmari, amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa matokeo ya utafiti wa uchumi pamoja na maeneo yanayostahili kushughulikiwa kwa haraka, utafiti uliofanywa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark.

Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Hebogard Jensen ni mmoja ya waliohudhuria hafla hiyo ambapo katika mahojiano na waandishi wa habari, balozi huyo amesema Tanzania ina fursa ya kufanya vizuri kiuchumi iwapo mkazo utawekwa kwenye sekta ya kilimo ambayo kwa sasa ndiyo inayoajiri watu wengi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT