Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Mizigo na Uchukuzi, Angelina Ngalula kwenye ufunguzi wa jukwaa hilo linalolenga kuangalia namna miundombinu iliyopo inavyoweza kuwanufaisha wananchi, wadau na Serikali.
Ngalula alisema Tanzania ina jiografia kubwa ya ushindani wa biashara kwa nchi jirani, hivyo uwapo wa ndege hizo na zitakazokuja inabidi uwe na manufaa makubwa kwa kushindana.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Faustin Kamuzora alisema Serikali ipo tayari kuwaunga mkono wadau hao kupitia jukwaa hilo kwa kushiriki mara kwa mara kujua changamoto na mapendekezo ambayo yatakuza sekta hiyo.
“Mara nyingi kitu ambacho hakijaandikwa huwezi kukifatilia, Serikali inayafanyia kazi maandiko yaliyojengewa hoja, pia takwimu nzuri ambazo zitafanyiwa kazi bila kipingamizi,” alisema Profesa Kamuzora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye alisema jukwaa hilo litakuwa ndio msaada wa kujua changamoto na namana ya kuisadia bandari ya Tanzania kupata faida na manufaa zaidi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT