Baraza la Waislamu nchini Marekani limemhimiza Donald Trump kuzingatia
haki na usawa wa wananchi wote bila ya ubaguzi wa kidini kufuatia
ushindi wake kwenye uchaguzi wa rais.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Washington, mkuu
wa baraza hilo Nihad Awad alitoa wito kwa rais huyo mpya kuzingatia haki
za wananchi wa Marekani wakiwemo Waislamu.
Akikumbushia matamshi ya chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu aliyotoa
Donald Trump wakati wa kampeni, Awad alisema, ''Waislamu wa Marekani
wataendelea kuishi nchini. Hatutoenda popote na wala hatutokaa kimya
kuhusu suala hili.''
Awad aliongezea kusema kuwa baraza hilo litaendelea kupigania haki za
Waislamu na uhuru wao kama ilivyokuwa hapo awali ili kumaliza
unyanyasaji.
Awad pia alitoa wito kwa Waislamu wote wanaoishi nchini humo kuondoa
hofu huku akiwakumbusha haki zao ambazo ni sawa na wananchi wengi wa
Marekani.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Donald Trump alikuwa akikshifiwa kwa
matamshi yake ya ubaguzi na kutaka kuzuia Waislamu kuingia Marekani huku
akitoa wito wa kufungwa kwa misikiti.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT