Mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya ombi la Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) la kuongeza bei ya nishati hiyo kwa wastani wa
asilimia zaidi ya 18.9 ifikapo mwaka 2017, unatarajia kuanza.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa wa Huduma za Nishati na
Maji (Ewura) imeeleza kuwa Oktoba 4, mamlaka hiyo ilipokea ombi la
mabadiliko ya bei ya umeme, hivyo unaandaliwa mkakati wa kukusanya maoni
ya wadau wa nishati hiyo.
“Mikutano ya ukusanyaji maoni kuhusu bei inayopendekezwa na Tanesco
itaanza Novemba 16 katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma na kwa
Dar es Salaam ni Novemba 23,” inaeleza taarifa hiyo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi saba tangu kutangazwa kwa bei mpya ya
umeme iliyokuwa na punguzo la asilimia 1.5 hadi 2.4 sanjali na kuondoa
tozo ya kuunganishiwa umeme ya Sh5,000 na gharama ya huduma kwa kila
mwezi ambayo ilikuwa na Sh5,520.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema shirika hilo
limefanya tathmini na kujiridhisha kuwa hakuna hasara itakayopatikana
endapo bei hiyo itatumika.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT