ALIYEKUWA Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amemlilia aliyekuwa
Spika wa Bunge la Tisa na mbunge mstaafu wa Jimbo la Urambo Mashariki
mkoani Tabota, Samuel Sitta, akisema Tanzania imepoteza kiongozi wa
mfano kwa vyama vyote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kafulila alisema Sitta alikuwa ni
kiongozi wa mfano kwa sababu ameacha mambo makubwa, ambayo aliyasimamia
bila kutetereshwa na mtu.
“Kwa kweli naweza kusema kwamba nchi yetu imepoteza kiongozi mkubwa
ambaye hakutetereshwa katika misimamo yake, ataendelea kukumbukwa katika
yale mambo ambayo aliyasimamia na yatabaki kwemye kumbukumbu za watu,”
alisema Kafulila.
Alisema Sitta ni mzee wake wa karibu na alimfanya kuwa sehemu ya familia
yake, hata kwenye sherehe ya Jubilei ya kutimiza miaka 50 ya ndoa,
alimualika kama mwanafamilia.
Aidha, alisema katika siasa, Sitta alijenga rekodi katika kusimamia
anachokiamini kwa muda mrefu, jambo ambalo ni nadra sana kwa viongozi
wengine na wazee wa taifa hili.
“Ndio maana alitofautiana na Rais wa Awamu ya Kwanza, Julius Nyerere,
Sitta akafukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pale, lakini hakubadili
msimamo wake na baadaye alirudishwa na kuchapwa viboko,” alieleza
Kafulila.
Alisema Sitta alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa, Rais mstaafu Jakaya
Kikwete alihutubia Bunge juu ya ufisadi, lakini Sitta akaonesha
kutofautiana naye bila kuwa na woga wowote.
“Kwa hiyo huyu ni kiongozi na mzee wa mfano, alikuwa anasimamia
anachoamini,” alisema Kafulila na kuongeza kuwa msiba huo ni mkubwa sana
katika mioyo ya watu wanaofahamu misimamo yake na pia kwa taifa.
Alisema Bunge la Tisa aliloliongoza, alitengeneza Kanuni za Bunge ambazo
zililifanya Bunge hilo kuwa lenye meno na la mfano, ambalo liliwafanya
watu wapende kulifuatilia.
Kafulila aliwataka vijana kusimama katika siasa alizokuwa, akiamini
Sitta kwani akiwa Spika wa Bunge, alifanya kazi vizuri na wabunge wa
upande wa wapinzani kwa usawa na aliwafanya wasikilizwe pamoja na
uchache wao bungeni.
“Ndio kanuni ya demokrasia, wengi waamue, lakini pia wachache wapewe nafasi ya kusikilizwa,” alisema Kafulila.
SOMA: ASKARI 152 WAFUKUZWA KAZI
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT