SIMBA SC imepunguza bei ya mchezaji Hassan Ramadhan Kessy kutoka Sh.
Bilioni 1.2 hadi Sh. Milioni 200 baada ya kikoa cha juzi ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo katika mkutano na
Waandishi wa Habari kwamba, japokuwa msuluhishi mteule, Mwenyekiti wa
zamani wa TFF enzi za FAT (Chama cha Soka Tanzania), Said El Maamry
hakuhudhuria, lakini kikao kilikwenda vizuri.
Lucas alisema kwamba Yanga iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wake,
Baraka Deusdedit, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Omar Said na Mawakili
Oscar Magolosa na Alex Mushumbusi, wakati Simba iliwakilishwa na
Mwenyekiti wake wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
“Kwa hali halisi ya uchumi kwa sasa, timu hizo zimezungumza hadi kufikia
mwafaka wa kiwango kisichozidi Sh milioni 200 kutoka dola 600,000
(zaidi ya Sh. Bilioni 1.2),”alisema Lucas na kuongeza; “Mazungumzo ya
wikiendi hii yanakwenda kukamilisha mvutano wao, kama ambavyo
walikubaliana kwenye kikao cha jana (juzi),”.
Katika kesi hiyo, Simba inamlalamikia Kessy kujiunga na Yanga kabla ya
kumaliza Mkataba wake, hivyo mchezaji amevunja Mkataba na anatakiwa
kulipa Sh. Bilioni 1.2 ambazo sasa zimeshushwa hadi Milioni 200.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT