Azam FC imeamua katika usajili wa dirisha dogo msimu huu kusajili
washambuliaji watatu kwa gharama yoyote ile ili kukiweka sawa kikosi
chao ambacho kipo nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Bara.
Makamu Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor ‘Father’, amesema vyovyote
itakavyokuwa lazima wakiimarishe zaidi kikosi chao kwenye usajili wa
dirisha dogo utakaoanza Novemba 15, mwaka huu.
Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 ambapo kwenye mechi 13,
imeshinda sita tu na kupoteza tatu ikiwa na sare nne, mwendo ambao
Father anaamini siyo wa kawaida kwa timu yao.
Tayari Kocha Zeben Hernandez amewataarifu viongozi wa Azam kuhakikisha
anaongezewa nguvu kwenye ushambuliaji ambapo Father amesema kuna sura
mpya tatu za washambuliaji watakaosajiliwa.
“Washambuliaji wawili watatoka nje ya nchi na mmoja wa hapahapa nchini,
tunataka kuhakikisha wanampa sapoti kubwa John Bocco katika kusaka
ushindi,” alisema Father.
Father amesema kuwa katika kutekeleza hilo, watamleta fowadi wao Mghana
Enock Ageyi ambaye anacheza Medeama kwa mkopo huku mikakati ya kusaka
straika mwingine wa kimataifa ikirarajiwa kuanza muda wowote.
“Kweli mikakati ya kuboresha kikosi ipo na kwa kuanza kocha ameomba
kuongezewa nguvu kwenye ushambuliaji. Mmoja tunataka awe mzawa na
mwingine wa kimataifa ambaye ataungana na Ageyi ambaye tulimuacha kwa
mkopo Medeama, naye anakuja ili kujaribu kumuongezea nguvu Bocco,”
alisema Father.
“Kwa ujio wa Ageyi tutakuwa na wachezaji wa kigeni zaidi ya kanuni,
hivyo lazima tumuache au tuwaache wengine ili kupisha hao wapya.”
Waivory Coast, beki kisiki, Pascal Wawa na Frasciso Zukumbariwa huenda
safari ikawakuta kutokana na mchango wao mdogo katika timu kwani Wawa
hajacheza mechi yoyote msimu huu ikidaiwa haelewani na Zeben.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT